Paul Pogba: Kipi kilichomuendea kombo mshindi huyu wa kombe la dunia pale Man Utd

Kipi kilichomuendea kombo mshindi huyu wa kombe la dunia pale Man Utd

Tue, 7 Jun 2022 Source: www.bbc.com

Paul Pogba alitoa hisia zake za jumla kuhusu muda wake aliokuwepo Manchester United kwa ustadi kabisa katika mahojiano ya hivi majuzi na gazeti la Ufaransa la Le Figaro.

"Lazima uwe mkweli, miaka mitano iliyopita haijaniridhisha - hata kidogo."

Alipofanya mahojiano hayo, ilikuwa chini ya miaka mitano tu tangu Pogba aifungie United bao katika ushindi wao wa fainali ya Ligi ya Europa dhidi ya Ajax.

Huo ulikuwa mwisho wa msimu wake wa kwanza tangu arejee Old Trafford, wakati United ilipolipa fedha za uhamisho uliovunja rekodi ya dunia ya wakati huo ya £89m kumrejesha mchezaji waliyekuwa naye katika akademi yao lakini wakampoteza kwa uhamisho wa bure kwenda Juventus baada ya Sir Alex Ferguson kukataa kumpa wakala mtata wa Pogba Mino Raiola uhakikisho wowote kuhusu muda ambao mchezaji huyo atapata uwanjani.

Lakini United hawajashinda taji lolote tangu wakati huo. Pogba anaondoka Old Trafford kwa mara ya pili, miaka sita kuu ya kiwango cha juu cha maisha yake ya soka katika klabu bila mafanikio.

Pogba ataondoka Man Utd kwa uhamisho huru

"Mwaka huu umepotea," alisema Pogba katika mahojiano yake ya hivi majuzi. "Hatutashinda chochote. Nataka kushinda mataji."

Kwani nini kilimuendea kombo Pogba?

Mkataba mnono

'Pogback', iikua bango katika video fupi katika mitandao ya kijamii ya klabu hiyo tarehe 9 Agosti, 2016. "Nimerejea," alisema Pogba, mwishoni mwa video fupi iliyotayarishwa kwa ustadi ya sekunde 26 kuthibitisha kuwasili kwake. Kwa ushirikiano na msanii wa rap wa Uingereza Stormzy pia, huu ulikuwa uhamisho wa uliovuma sana na wa gharama sana.

Ukweli pia Pogba alikuwa mmoja wa wanamichezo mashuhuri zaidi wa Adidas na alikuwa akisaini mkataba na United, ambao walikuwa na miezi 12 tu katika mkataba wao wa miaka 10 na gwiji huyo wa nguo za michezo wa Ujerumani, ulimaanisha kuwa uhamisho wake ulikuwa wa maana kubwa kibiashara.

Meneja mpya Jose Mourinho alimtaka. Na kwa mtendaji mkuu Ed Woodward, kuanza kuhisi kiti cha moto baada ya kuwatimua mameneja wawili, ilikuwa na maana pia.

Hii ilikuwa nafasi ya kurekebisha makosa ya Ferguson, ili kuthibitisha kwamba United inaweza kuvutia wachezaji wa hadhi ya juu na kumrejesha mhitimu wake huyo wa kituo chake cha vipaji cha watoto.

Hata hivyo, kulikuwa na gharama kubwa ya kulipa. Raiola alikuwa mwerevu kwenye mipango ya usajili.

Kulingana na taarifa zilizowekwa hadharani na tovuti ya Football Leaks, ambayo haijawahi kupingwa na Old Trafford, kandarasi ya Pogba ilikuwa ya pauni milioni 7.75 kwa mwaka. Bonasi ya uaminifu ya £3.75m kwa mwaka pia ilijumuishwa. Ikiwa United ilifuzu kwa Ligi ya Mabingwa, Pogba aliweka kibindoni zaidi ya pauni milioni 1.85. Aidha, Pogba alikuwa na mkataba wa haki ya picha wa £3m kwa mwaka. Raiola mwenyewe alilipwa fedha ya kushangaza kiasi cha £41m.

Utamchezesha wapi pogba?

Hili bado ni jambo la kustaajabisha, lakini ukirejea wakati wa Pogba akiwa United, hakuna mstari thabiti wa mahali Pogba anafaa kutumika.

Anawez akuwa sehemu ya kiungo cha kati cha watu wawili? Upande wa kushoto wa viungo watatu? Kama namba 10? Au mbele kama mmoja wa washambuliaji wawili wa juu?

Ni dhahiri kwamba hata akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa - ambayo alishinda nayo Kombe la Dunia la mwaka 2018 - uwezo wa Pogba unaonekana katika eneo la ushambuliaji. Umiliki na upigaji wake pasi ni wa kiwango cha dunia. Akitokea katikati anakuwa hatari zaidi. Lakini anahitaji kusaidiwa mahali anapotoka, kwa sababu anaweza kupwaya linapokuja suala la ulinzi.

Hata hivyo katika msimu huo wa kwanza, Pogba alipopewa uhuru wa kucheza atakavyo mbele, mara nyingi Zlatan Ibrahimovic alikuwa akirudi kwenye nafasi zile zile ambazo Mfaransa huyo alitaka kuzitumia.

Wakati huo, ilionekana kama tatizo na kitu ambacho kingetatuliwa kwa kawaida kutokana na umri wa Msweden huyo ulimaanisha kuwa hangeweza kuwa mchezaji mwenza wa Pogba kwa muda mrefu.

Lakini United hawakupata suluhu la kutosha. Hata bila Ibrahimovic, wachezaji wao wakubwa wasumbufu: Anthony Martial, Marcus Rashford na Jadon Sancho, walipenda kufanya kazi katika maeneo yale yale ambapo Pogba anafanya vyema.

Iwapo angeshuka sana, iliiathiri safu ya kiungo ya United. Uwezo wa Freed na Scott McTominay umedhihakiwa, hawakaribii kipaji cha Pogba.

"Ni rahisi nikiwa na timu ya taifa Ufaransa, nacheza na ninacheza katika nafasi yangu - najua jukumu langu na ninahisi kujiamini kwa kocha na wachezaji," Pogba aliiambia Le Figaro. "Ni kawaida kuhisi tofauti pale Manchester United kwa sababu ni vigumu kuwa na kiwango bora endelevu wakati mara nyingi unabadilishwa nafasi ya kuchgeza, au mfumo wa timu, au wachezaji wenzako."

Mwisho wa kusikitisha

Katika mechi yake ya mwisho, Pogba alitolewa nje na kukejeliwa na mashabiki wa United.

Pogba amecheza mechi 20 za ligi kuu katika msimu wake wa mwisho akiwa mchezaji wa United. Alifunga mara moja tu - dhidi ya Burnley - na kutoa pasi za mabao tisa. Pasi nne kati ya hizo zilikuja kwenye mchezo wa ufunguzi dhidi ya Leeds.

Mechi hiyo iliyopigwa Old Trafford ni moja kati ya nyakati bora za Pogba kung'ara United. Ushindi maarufu wa 3-2 wa kurejea Manchester City mnamo 2018, alipofunga mara mbili, ulikuwa mwingine. Fainali hiyo ya Ligi ya Europa dhidi ya Ajax na mshindi wake wa goli akiwa Burnley misimu miwili iliyopita walikuwa wengine.

Lakini zilikuwa za muda mfupi. Kila kukosekana kwa jeraha kulikuja na tuhuma miongoni mwa baadhi ya mashabiki kwamba Pogba hataki tena kuichezea klabu hiyo.

Alipotoka uwanjani baada ya mechi yake ya mwisho Man United, dhidi ya Liverpool mwezi Aprili, alizomewa na mashabiki wa timu hiyo.

Safari imeishia hapo.

Source: www.bbc.com